
Everton wakataa kumsajili Coady
Everton wameamua kutochukua chaguo la pauni milioni 4.5 kubadilisha uhamisho wa mkopo wa muda mrefu wa mlinzi Conor Coady kutoka Wolves hadi uhamisho wa kudumu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alicheza mechi 25 akiwa na The Toffees na kufunga mabao mawili.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alianza kuichezea Everton ilipoilaza Bournemouth 1-0 siku ya mwisho ya msimu na kujihakikishia kiwango cha juu.
Hata hivyo, alicheza mara sita pekee chini ya bosi wa Everton Sean Dyche, ambaye alichukua mikoba ya Goodison Park mwishoni mwa Januari.
Everton pia imethibitisha kuwa beki wake Ruben Vinagre atarejea Sporting Lisbon kufuatia muda wake wa mkopo katika klabu hiyo.
"Tunataka kuwashukuru kwa dhati Conor na Ruben kwa weledi wao mzuri na mchango wao muhimu ndani na nje ya uwanja wakati wao wakiwa na klabu," alisema mkurugenzi wa soka wa Everton Kevin Thelwell.